
Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries aliwahi kuandikwa
sana na vyombo vya habari duniani kwa kuwaagiza wafuasi wake kula majani
kama wanyama kwa madai kuwa binadamu wanaweza kula chochote kilichotoka
kwa Mungu.
Kitendo hicho kiliwaacha waumini wengi wakitapika na kuharisha. Na
sasa anawataka waumini wake kunywa petroli kwa madai kuwa itageuka kuwa
juice ya nanasi.