Binadamu wamepoteza utu! Mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa jina la mama Janeth, mkazi wa Kimara-Suka jijini Dar anadaiwa kujifungua kisha kukiweka kichanga kwenye begi na kukitupa shambani, kisa kikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi na mwanaume aliyempa ujauzito.
Mama anadaiwa kutupa kichanga hicho akijaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamuona alifahamika kwa jina la mama Janeth.
Mmoja wa mashuhuda akizungumza na gazeti hili, alisema kichanga hicho kilikutwa na bibi anayejulikana kwa jina la mama Joyce katika shamba lake lililopo eneo la Moa, Kimara-Suka baada ya kubanwa sana mama Janeth alikiri kuwa ndiye mwenye kichanga hicho.