Showing posts with label ukatili. Show all posts
Showing posts with label ukatili. Show all posts
Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi

Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi

Mtu mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.

Kamugisha alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti 2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa kimapenzi.

Aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia wakati wakipigana.
UKATILI..!! MUME AMNYONGA MKEWE, KISA WIVU WA MAPENZI!

UKATILI..!! MUME AMNYONGA MKEWE, KISA WIVU WA MAPENZI!

Stori: Waandishi Wetu INAUMA sana! Katika kinachoonekana kama ni wivu wa kimapenzi, dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Magdalena Lucas ( 23) ameuawa kikatili na ‘mumewe’ aliyetajwa kwa jina la Stephano Lucas (28) nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam wiki iliyopita baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kufungiwa chumbani kwa siku tatu.
Mama Atupa kichanga......Alikiweka Kwenye Begi Kisha Kukitelekeza Shambani...Kisa Ugomvi wa Mapenzi!

Mama Atupa kichanga......Alikiweka Kwenye Begi Kisha Kukitelekeza Shambani...Kisa Ugomvi wa Mapenzi!

Binadamu wamepoteza utu! Mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa jina la mama Janeth, mkazi wa Kimara-Suka jijini Dar anadaiwa kujifungua kisha kukiweka kichanga kwenye begi na kukitupa shambani, kisa kikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi na mwanaume aliyempa ujauzito.
Mama anadaiwa kutupa kichanga hicho akijaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamuona alifahamika kwa jina la mama Janeth.
Mmoja wa mashuhuda akizungumza na gazeti hili, alisema kichanga hicho kilikutwa na bibi  anayejulikana kwa jina la mama Joyce katika shamba lake lililopo eneo la Moa, Kimara-Suka baada ya kubanwa sana mama Janeth alikiri kuwa ndiye mwenye kichanga hicho.

MENGI ZAIDI YA SAKATA LA VIDEO YA HOUSEGIRL ALIYEMTESA MTOTO WA MIAKA MIWILI KARIBU YA KUUA...!!!


Habari iliyotingisha na kuhuzunisha wengi jana ni ile video inaonesha mtoto aliyekuwa akiteswa karibu kufa na msichana wa kazi huko Uganda. 

Video hiyo iliyosambaa mitandaoni ikionyesha jinsi msichana huyo wa kazi alivyokuwa akimfanyia ukatili wa kinyama mtoto wa miaka miwili, video hiyo ilionyesha mateso ya kipigo na pia jinsi alivyokuwa akimlazimisha mtoto kula chakula kwa namna ya kikatili. Habari zinasema baba wa mtoto huyo aliamua kuweka kamera ya siri nyumbani hapo, baada ya kuona mtoto hakuwa na hali ya kawaida, na kwamba alikuwa anaonyesha dalili za unyonge na woga kwa msichana wa kazi. Habari zinasema mzazi huyo hakuamini alichokiona na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kumvamia msichana huyo na kumpa kipigo kitakatifu,mpaka majirani walipoingilia kati, na kumuokoa msichana huyo wa kazi


UMEIONA HII VIDEO NZIMA YA HUYU DADA WA KAZI ANAVYO MTESA HUYU MTOTO?

Kama kutakuwa na list ya watu wasio kuwa na huruma hata kidogo ama kwa lugha nyingine tunaweza kusema katili basi bila shaka huyu dada wa kazi kwenye top 10 atashika nafasi ya kwanza…
Hii inawahusu sana wakina mama ambao uwaachia watoto wao Dada wa nyumbani (HOUSE GIRL) pengine kutokana na majukumu ya kikazi au inapotokea safari ya ghafla… hii video itakuonesha tukio zima na tabiwa kama hii wapo baadhi ya Madada wanazo ivyo umakini mkubwa unatakiwa.