RAY: SIO LAZIMA NIFAHAM KINGEREZA KWANI ATA WATU MAARUFU UKO ULAYA AWAJUI KINGEREZA



Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live

kinachokukutanisha na watu mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane kamili.
SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA
Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya kiingereza.
Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.
CHUCHU MCHUMBA WANGU

Msanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika kuwa yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae anafahamika kama Chuchu Hansi hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli jamaa anampango wa kumuoa binti huyo au laah,na majibu ya Ray uyalikuwa kwamba wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote juu ya suala hilo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »