
"Kujichubua ndio Habari ya Mjini ...Haha Hako kamsemo nakasikia sana mitaani kutoka kwa wasichana na kweli ukiangalia wasichana Wengi hasa mastaa wetu hapa Bongo Wamejichubua Ngozi na kuonekana Weupe..Mie siwakatazi ila nawapa Onyo tu ,
Ukiamua kujichubua basi tumia Vipodozi Sahihi na ambavyo vimeshajaribiwa , Wengi Wanatumia Mikorogo ya Mitaani ambayo madhara yake ni kama unavyoona kwenye picha hapo juuu, na wengine wamejichubua na kushindwa kuendelea kutumia dawa sahiii ambazo ni ghali hivyo kugeukia migorogo ya mitaani ama kuacha kabisa na ngozi yao kugeuka kuwa kama ya chura ..Hao mastaa waliojichubua wanahela za kumaintain mikorogo ya Ukweli ..Kama hujajichubua ni bora usifanye hivyo..Tafuta vipodozi vitakavyo ng'arisha ngozi yako lakini si kujichubua"