Wema na Diamond
Meninah
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media nyinmgine kuziandika kwa kasi.
Meninah Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kuwa Wema ametoswa sababu ya kuendekeza pombe inayompelekea kuwa mvivu na kutotaka kufanya kazi badala yake ni starehe tupu, kwa maana kuwa hata nyumbani kwa mama Diamond haendi mara kwa mara kumsalimia inaweza hata kupita miezi 3 hajaenda ila Meninah anaenda na akifika kule humsaidia mama Diamond kazi, kupika na kupakua. Chanzo hicho kimesema kuwa hata Wema anajua kuwa Diamond na Meninah wana ishara zote za kuwa wapenzi lakini hana cha kufanya, huku Meninah yeye akiwa tayari amejitoa muhanga kwa Diamond lakini anawaogopa Team Wema kumshambulia hasa kwa mvua za matusi kama ilivyo kawaida yao lakini mama Diamond anampoza kuwa asiwe na shaka yeye kamkubali Diamond hawezi kukataa kumuoa hilo amuachie yeye mama Diamond.
Vikao hivyo licha ya kuhudhuriwa na mama Diamond na Queen Darleen, chanzo hicho kimesema pia kuwa kuna ndugu wengine wa Diamond na mama Diamond wanahudhuria ila yeye hawajui sababu hana ukaribu nao.