
Mrembo baada ya kuuawa.
DADA mmoja anayedaiwa kuwa mkazi wa jijini Dar es Salaam ameuawa kinyama baada ya kubakwa na vidume wanne hadi kufa eneo la Nanenane ndani ya mashamba ya mikonge mjini hapa.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, mrembo huyo ambaye hakufahamika aliuawa kwa kubakwa na watu wasiojulikana ambapo maiti yake ilikutwa ikiwa imevuliwa nguo za ndani
Aidha, kwenye shingo yake kulikutwa na kitambaa ambacho inadhaniwa kuwa ndicho kilichotumika na wauaji hao