Uhaba wa Wanaume: Msichana Mrembo Aamua "Kujioa Yeye Mwenyewe" Baada ya Kukosa Mume.

Uvumilivu wa kusubiri mwanaume wa kuja kumpigia goti na kumuuliza ‘will you marry me?’, umemshinda mwanamke mmoja wa Uingereza, aliyeamua kuchukua uamuzi wa kujichumbia na kujioa mwenyewe!

Grace Gelder ambaye ni ‘mme na mke’ alijichumbia November, 2013 na baadae kujioa March, 2014 na kuamua kufanya sherehe ya harusi yake iliyohudhuriwa na wageni 50.



Na ule wakati wa ile hatua ya ‘you may now kiss the bride’ ulipowadia, Grace alijibusu kwenye kioo.
Mwanamke huyo alisema baada ya kuwa single kwa miaka 6 aliamua ku-fall in love na ‘yeye mwenyewe’ baada ya kuona hapati mtu wa kumpenda.

Mwanamke huyo alisema kuwa pia wimbo wa Björk song Isobel ambao una mstari unaosema ‘My name’s Isobel, married to myself’, nao ulimuhamasisha kutimiza azimio lake.

1.Sasa mie nashangaa, hivi wanaume wa kuoa wameisha ulimwengu huu??? 
2.Je, ndio kusema wanaume domo zege ndo wanazid ongezeka duniani kila kuchao?
3.Je, ndio kusema mabinti wa kileo ndo wanazidi kuchuja /kukosa mvuto wa kuolewa?
4.Je, ni kitu gani mabinti warembo wanakosea mpaka kufikia hatua hii ya kujioa mwenyewe?

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »