Wakati mwingne wanaume au watu tofauti
hudhani kwamba, wanawake wanaovaa
nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa
sababuya kutafuta soko kwa wanaume.
Inawezekana kukawa na wale ambao wana
sababu hizo, lakini wapo wale ambao
wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao
kwamba wanamapungufu kwa mfano sura
zao zimewaangusha, hivyo miguu yao
mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu
huo.
Wakati mwingine hata wanawake
wanaodhani au kudhaniwa kuwa niwazuri,
wamekuwa wakivaa nguo fupi
zinazoonyesha maungo yao.Hawa nao ni
lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani
Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa
zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa
wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na
kutoolewa kwao, bado wao wana sura na
miguu au miili mizuri.
Udhaifu wowote ambao unamkera
mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au
kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza
kuonyeshwa kwa mwanamke huyo
kuyatangaza yalemaeneo ya mwili wake
ambayo anaamini ni mazuri.
Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa
kuamini kwamba bado anayo thamani,
kwani ataangaliwa sana na wanaume,
kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa
nguo za kubana huku wakiwa na makalio
makubwa...
Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao
au wengi huamini kwamba ni mbaya.
Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba,
pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni
wazuri sana katika maeneo mengine ya
mwili ambayo wanaume na hata
wanawake wengi huyapenda au kutamani
kuwa nayo.