Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga
amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato
Mkoani Geita.
Mheshimiwa
Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie
Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari
ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye
kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao
Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na
familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao,
kwa lengo la kumsalimia.
"Nimekuja
kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja
kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa
Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato" Alisema Mheshimiwa Odinga.
Pamoja
na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais
Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa
wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake
Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akikumbatiana na Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada
ya kuwasili nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
Waziri
Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais John Magufuli, Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga Bi. Ida
Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani
Geita.
Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na mama mzazi wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara baada ya
kuwasili Chato Mkoani Geita.