MAAJABU ::JIONEE PICHA AJIFUNGUA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 5 NDIE MWANAMKE MDOGO DUNIANI KUJIFUNGUA


     Lina Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.
Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliye mpa jina la Gerardo Medina. 
Ilianzaje? Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7. Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito. 
Alizaaje? Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo. Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta. 
Alivunja Ungo lini? Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse Médicale. Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3. Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka. 
Alizaa mtoto gani? Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.
Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.
Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.
Nani Baba wa mtoto? Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba. Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kua hakutoa majibu yanayo jitosheleza. 
Tuhuma kwa baba mzazi: Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza. Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana 
Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na Raúl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume. Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru

je unalitambua hili?: Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume.


Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako. Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote.
  Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi! Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa. Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini 
Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani? Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. 
Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi

Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi

Mtu mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.

Kamugisha alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti 2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa kimapenzi.

Aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia wakati wakipigana.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt JOHN MAGUFULI Nyumbani Kwake CHATO

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.