Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt JOHN MAGUFULI Nyumbani Kwake CHATO

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
PICHA: UTEKAJI WATOTO WATIKISA KUWAVIZIA WAKITOKA SHULE, POLISI WAFYATUA RISASI KUWATAWANYA WANANCHI - DAR

PICHA: UTEKAJI WATOTO WATIKISA KUWAVIZIA WAKITOKA SHULE, POLISI WAFYATUA RISASI KUWATAWANYA WANANCHI - DAR

Stori: Makongoro Oging’
MUNGU wangu! Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura nyingine.

Wanafunzi wa shule ya msingi wakitoka madarasani baada kutokea kwa hali ya vurugu.

Safari hii, gari moja lilitupiwa mawe na dereva nusura kuuawa kufuatia kufika katika Shule za Msingi za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar kwa lengo la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo lakini likahofiwa lilikwenda kuteka watoto.
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita na kusababisha vurugu kubwa kati ya wazazi na walimu hali iliyowafanya maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni kuwasili katika eneo la tukio ili kutuliza ghasia na kwanusuru walimu.
KIJANA ZINGATIA HILI:HIZI NDIZO MBINU ZA KUISHI KAMA HAUNA PESA MFUKONI !!!!.

KIJANA ZINGATIA HILI:HIZI NDIZO MBINU ZA KUISHI KAMA HAUNA PESA MFUKONI !!!!.


Na James Mwang'amba
WAZUNGU wana msemo wao unaosema, ‘Life is unpredictable’ wakimaanisha kwamba maisha hayatabiriki. Wapo ambao walikuwa na hali nzuri sana kifedha huko nyuma lakini leo hii ukiwaona huwezi kuamini. 
Wanaishi maisha magumu sana tena kwa msaada wa watu wengine. Hayo ndio maisha! Leo hii ukiwa juu usijipe asilimia mia moja kwamba siku zote utakuwa juu. Upo uwezekano mkubwa kabisa wa siku moja kuwa chini na waliokuwa chini wakapanda.
Kwa mantiki hiyo basi tunapolizungumzia suala la kuishiwa linamgusa kila mtu bila kujali tajiri wala maskini. Kimsingi kuishiwa ni hali ya kukosa pesa kwa ajili ya matumizi yetu ya kila siku.
Hali hii ni ya kawaida katika maisha ya binadamu. Hii inamaanisha kwamba unaweza ukawa unafanya kazi na kuwa na kipato kizuri tu, lakini katika mazingira fulani ukajikuta pesa ambayo ulikuwa nayo imekwisha. 
Yawezekana ukawa umepata matatizo yanayohitaji fedha nyingi ukazitumia katika kutatulia matatizo hayo au unaweza kujikuta umeishiwa baada ya mshahara kuchelewa na ukajikuta kwamba huna kitu kabisa.

SAD NEWS: Profesa UDSM auawa kwa risasi Dar....soma zaidi hapa


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana.

Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.