Penny na Wema
Penny ameshare picha kwenye Instagram akiwa pamoja na Miss Tanzania huyo wa zamani ambayo Wema pia ameirepost kwenye akaunti yake. Hiyo ni picha ya kwanza ya warembo hao wakiwa pamoja kuwahi kuweka kwenye akaunti zao katika kipindi kirefu.
Wakiongea kwa pamoja na Bongo5 leo wakifanya shopping ya nguo, warembo hao wamedai kuwa wana mipango ya kufanya filamu pamoja na wanatarajia kuingia kambini mwakani.
Picha hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wao wanaopenda kuwaona wakiwa pamoja.