Simu za Nokia ni moja ya simu ambazo zimekuwa na umaarufu mkubwa Duniani, mbali na hiyo hii ni moja ya Kampuni kongwe zaidi kwenye soko la bidhaa hizo.
Kuna wakati ambao umaarufu wa bidhaa za Nokia ulishuka, lakini unaambiwa kwa sasa wanakuja hivi; Nokia wametengeneza simu za Nokia 215, zitakuwa za line moja na line mbili.
Wanakadiriwa kwamba zikiingia sokoni bei yake itakuwa ni dola 29, ambayo ni sawa na sh. elfu 50 kwa T’zania.
Microsoft wamepanga kuiuza simu hii Afrika, Asia, Ulaya, na Mashariki ya Kati japo hawajasema lini itakuwa sokoni.
Hii ni moja ya hatua kubwa ambazo Nokia imezipiga sokoni tangu Kampuni hiyo inunuliwe na Microsoft.